ENDELEA...............
..................Nilikaa nikawa najiuliza maswali mengi sana ambayo hayana majibu. Swali kubwa ni kujua wapi naelekea?. Siku ya mwisho ni pale nilipoona sitaki kwenda kwa hao jamaa yani kumfanyia kazi tena bwana Paul nitapambana mimi mwenyewe ili nimlinde mwanangu. Niliona haina haja sana ya kujiuliza nilichomoka pale na kwenda sasa muda muafaka wa kwenda kuanza kazi kwa nguvu zangu zote.
Niliandaa kila kitu huku nikiwa sina habari yeyote ile, hakika siku hiyo bahari ilikuwa shwari sana yani tulivu zaidi ya maelezo. Niliweka mashine ya kusukumia mtumbwi wangu kisha nikaelekea mbali sana ya bahari nikipita kuangalia sasa maeneo mengine ya kuwapata samaki. Nilichokuwa nakifanya ni kumwaga matunda fulani ambayo huwa wanayapenda sana samaki kula.
Nilimwaga nyingi kiasi kwamba wale samaki pale wazoee. Nilipohakikisha kuwa tayari ndipo nikasonga mbele zaidi kama unavyojua bahari ni kubwa sana. Niliendelea mpaka nikahisi kama napotea.
Niligeuza Boti kwa ajii ya kurudi nyumbani sasa. Wakati nageuza ndipo nikakiona kisiwa kwa mbali, nilijiuliza kuwa yale maeneo sikuwahi kwenda kabla ila leo nimepaona sasa ngoja siku nyingine nitafika kule.
Nilitembea taratiibu kurudi huku nikisikiliza nyimbo za wasanii wetu wa bongo hapa. Nilikuwa napenda sana kusikiliza ngoma za bongo kwa kuwa ndizo zilikuwa zinanifanya nijisikie nafuu sana.
Simu yangu iliita kuashiria kuwa kuna mtu ana piga hakuwa mwingine alikuwa bwana Paul. Nilimpotezea kabisa. Alipiga tena ndipo nikapokea simu yake.
"Mnali!!"
"Ndio mimi unasemaje?"
"Mnali, unaongea na mimi hivyo!!"
"Kwani nini unanifuatilia sana jamanii tafuteni watu wengine wenye digilii zao za uvuvi mimi sitaki"
"Sawa basi fungua watsapp sasa hivi kuna ujumbe mfupi naamini utakufurahisha sana.."
"Usinitisheee nakuambia usiniti....shee"
Bwana Paul akakata simu.
Nilitamani ile simu kuitupia ndani ya maji lakini niliona vyema kwanza niangalie ule ujumbe ambao kaniambia.
Pale nilipo mtandao ulikuwa unasumbua sana hivyo sikuwa na papara sana kwanza alishanichanganya.
Nilitembea lakini kwa mbali nikahisi kama mlio wa boti ukinifuata kwa kasi mbele yangu. Ilinibidi nisimame kwanza ndipo nijue kuna jambo gani kabla hata haujachukua hatua yeyote. Nililiona kweli linakuja kwa kasi zote nilichuchumaa kisha nikageuza kuelekea upande mwingine japo haikuwazuia wao kutonifuata.
Hatimae walinikaribia pale nilipo wakiwa na ile spika ya kutangazia matangazo.
Wakiwa kwa mbali walisema kwa sauti iliyonifanya mimi kusikia
"Mnalii, umekataa agizo la tajiri yetu na kumfanya apoteze wateja wengi kwa ajili yako...sasa tunakupa dakika tatu za kusali ili tukupoteze kabisa". Walinisogelea hadi pale nilipo na ndipo wakawa wananitisha sana. Sikuweza kuona sura zao.
Nilipatwa na wasiwasi sana baada ya ile kauli ambayo wameitoa mbele yangu. Nikawa najiuliza wametumwa kuniua kwa lipi?. Hata sikuweza kusema ndipo nilishtukia tu kitu kimekita kwenye Boti yangu alafu ikatoboa sikujua kitu gani nilichoshangaa ni sauti pamoja na mtumbwi kupitisha maji tu.
Maji yalizidi kuingia ndipo wale watu waliondoka nilisimama na kuinua mikono juu ili hata wanione lakini haikusaidia.
Nilibaki kupakua yale maji ili yatoke maji yalikuwa yanaingia kwa kasi sana
Kila yalipokuwa yanazidi kuingia ndani na mimi ndipo niilipokuwa nachanganyikiwa zaidi na kama kama kuogelea ndio lakini siwezi kwa ule umbali wote ambao nilikuwa kutoka nchi kavu. Mtoto wa kiume hofu iliingia zaidi ya maelezo japo na ukubwa wangu lakini chozi lilianza kujitokeza bila hata kulitaka.
Nilifanya kazi ya kupakua lakini nguvu ziliniishia . Ajabu zaidi mvua ilionekana kuanza hatimae mvua kubwa ikaanza kupiga pale, sikuwa na hata la kufanya zaidi ya kusubiria kifo ndicho ambacho kilibakia. Nakumbuka kauli yangu ya mwisho pale ni kuwa Kama nimewafanyia dhulma basi naomba msamaha ili nikifa niwe huru.
Hii yote kutokana na kutapatapa tu bila hata mpango kwa kuwa kifo kipo mbele yangu. Mawimbi makubwa yalizidi kunipeleka tofauti na mimi ninakotaka kwenda.
Yalinisukuma upande ule ambako nilitoka. Hofu ilitanda sikujua nifanye jambo gani ili kujinasua na lile swala ambalo linaendelea pale. Hatimae wimbi likanipiga na kujaza maji mule nilimo, daah!.
Mengine yalikuwa yanaingia mvua inazidi na mawimbi pia yalizidi kuniyumbisha hatimae nauona kabisa unazama nikajiokoa kwa kuruka na kuanza kupiga mbizi ambazo hazikuleta matumaini kabisa kwani, nilichoka kwa haraka sana.
Ma ya bahari ni tofauti kabisa na ya mto na mengine. Maji ya bahari ni yenye chumvi sana kwa wale wasioyajua.Yaliingia mdomoni puani nikashindwa kuhema.
Kilichoendelea pale sikuwa nafahamu kabisa kwani nilizimia yani.
Muda nashituka toka usingizi wa kifo ni usiku. Nilihisi tumbo kujaa, kifua nacho kujaa niliinuka nashindwa nguvu zimeniishia. Sikujua ni mahali gani pale nilipo kabisa kwa kuwa mazingira ni ya usiku ila kilichonijulisha kuwa sipo kwenye maji ni mchanga ambao nilikuwa nimeushika mikononi mwangu huku nikiwa nimelala chali.
Nilikohoa ndipo nikatapika maji kwa wingi sana, niliendelea kutapika hivyohivyo mpaka pale nilipopata nguvu ya kuinuka.
Usiku mkubwa sana na mazingira yalinitisha kwani sikufahamu. Nilisimama huku nikiwa nayumbayumba tu. Mbele niliwaona kama watu wawili wamesimama.
Nilijitahidi kutoa sauti nikashindwa kbisa kutoa. Nilivuta kumbukumbu hakika sikuwa nakumbuka kitu nikawa kama nimezaliwa upya kabisa.
Kwa kuwa nilikuwa tofauti kabisa pale. Nilishindwa kuwafuata wale watu ndipo nikaanguka chini na kushindwa kabisa kufanya jambo lolote lile pale.
Asubuhi na mapema sana jua likiwa limechanua na kuwa ng'avu niliinuka. Mbele yangu nilipoangalia naona nyayo za simba mnyama ambae hana mzaha kabisa, lakini si nyayo za simba tu ila pia na za binadamu zipo pale, nikajishtukia baada ya akili yangu kurudi kuwa nilipo sio pale ambapo nastahiki. Nikajua labda nimekuja na mtumbwi wangu kumbe hapana sijui hata nimefikaje pale.
Nikakimbia kuelekea karibu na maji nashangaa nimefikaje lile eneo. Nikavuta picha ndipo nikagundua kuwa ni pale kisiwani ambapo nilipaona jana yake.
"Eeeeeh! Mama yangu hapa ni sehemu gani, na nimefikaje sasa, aaah! Mh! Mbona haya majaribu sasa je? Hizi nyayo za watu nibwatu wa aina gani wanaishi huku je? Na wao ni wavuvi kama mimi au je? Wanafanya kazi gani."
Nilibaki kujiuliza huku nikiwa nimeshika kichwa changu na mikono kama mtu ambae kafiwa na wazazi wake wote.
Nilijipa moyo baada ya kuona zile nyayo nikajitahidi kwenda kuanza kuzunguka kile kisiwa nijue kuna jambo gani hasa lipo mule. Niliingia zaidi kuzunguka kile kisiwa sikuona hata pakuanzia kuingia ndani.
Wakati nazidi kuangalia ndipo nikawashuhudia watu kama watatu wakiwa wanakula nyama ya mnyama daah! Kilichonishangaza ni maumbile ya wale watu. Vichwa vyao ni vidogo sana kiasi kama ngumi mbili zilizounganishwa. Hawakuniona kabisa. Niliendelea kuwaangalia ndipo nikatikisa mguu wangu kutokana na kutokuwa na nguvu maana ulikuwa umechoka sana. Waligeuka nyuma wakapiga kelele.
""Nyaaaaaaa nyaaaaaa""".
Wakanisogelea kha! Japo nguvu sikuwa nazo nilikimbia huku wakinifuata kwa nyuma niliposhindwa nikajirusha kwenye maji baada ya kuhisi kuwa na udogo wao hawatoweza kuingia.
Niliwashangaa wanarudi huku wakirukaruka yale maji na upiga kelele.
Walikaa pembezoni kabisa na mahali panapoishia maji wakinisubiri ndio ikawa afueni yangu pale.
TUKUTANE TOLEO LIJALO




No comments:
Post a Comment